Mhe. Mstahiki Meya na wajumbe wa kamati ya fedha na wakuu wa idara wakikagua ujenzi wa barabara unaoendelea katika mtaa wa Kingo mkoani Morogoro.
AMIRI JUMA NONDO
Mhe -Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na Diwani wa Kata ya Boma-2010/2015
Wednesday, 23 July 2014
Friday, 11 July 2014
Meya Amiri Juma Nondo ndani ya UN headquarters kwenye mkutano wa kuzungumzia maendeleo endelevu ya miji , manispaa na majiji.

Thursday, 10 July 2014
Barabara za Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami kuanzia mwaka wa fedha. Hizi ni juhudi na umoja kati ya Baraza la Madiwani linaloongozwa na Mstahiki Meya Mh. Amiri J. Nondo na Mkurugenzi wa Manispaa na timu yake ya watendaji. Nia na madhumuni ni kuhakikisha wananchi na wakazi wa Morogoro wanapata huduma iliyobora na kuipelekea Manispaa kuwa jiji.

Mwonekano wa mbele wa ujenzi jengo la Hosipitali ya Wilaya kata ya Kihonda.

Mstahiki Meya Mh. Amiri J. Nondo akifungua na kuongea na Wakandarasi walioshinda Zabuni ya Ujenzi wa Barabara ambapo katika Hafla hiyo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro amesisitiza kuwa ujenzi huu utafanyika kwa kiwango cha Lami katika barabara zake zilizopo katikati ya mji na pembezoni. Katika hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Viongozi wa Chama Tawala CCM ikiwa ni moja ya juhudi za kufuatilia ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh. Amiri J. Nondo akiwa na waheshimiwa Madiwa na wakuu wa Idara katika ukaguzi wa ujenzi wa Hosipitali ya Wilaya inayojengwa kata ya Kihonda. Ujenzi huu wa Hosipitali ni awamu ya kwanza hivyo itakua ikitoa huduma kwa wagonjwa wa nje "Out patients". Hizi zote ni juhudi za Mstahiki Meya pamoja na baraza la Madiwani na Mkurugenzi Wa Manispaa ya MorogoroBw Jervis A. Simbeye pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo katika kuboresha huduma ya afya ndani ya Manispaa ya Morogoro.Jengo hili litakabidhiwa hivi karibuni.

Monday, 7 July 2014
Welcome
Furahia kuperuzi mambo mbalimbali ya Morogoro , Ndani na nje ya Nchi katika nyanja mbalimbali ,nataraji kupokea mawazo na ushauri toka kwako juu ya kile nitakachowasilisha , AKHSANTE
Karibu sana ...................................;
Subscribe to:
Posts (Atom)